Wq/sw/Ibrahim Hamis Juma

From Wikimedia Incubator
< Wq‎ | sw
Wq > sw > Ibrahim Hamis Juma

Ibrahim Hamis Juma (amezaliwa 15 Juni 1958) ni wakili Mtanzania na Jaji Mkuu wa sasa wa Tanzania.[1]

Nukuu[edit | edit source]

  • Nchi zilizoendelea tayari zimeona wingu zito la mabadiliko linalonyemelea, na wao tayari wamegundua na kuona kuwa ujuzi uliopo, kazi nyingi na biashara nyingi ambazo wananchi wao walizosomea, kuhitimu na kupata ajira, zinatoweka kwa sababu Dunia kwa sasa inasukumwa na Mapinduzi ya Nne ya Viwanda (4IR).[2]
  • Sekta ya Umma ina nafasi na uwezo mkubwa wa kuibua fursa za kibiashara, uwekezaji ambazo zinaweza kuwawezesha Mawakili kushiriki katika Sekta Binafsi hasa katika maeneo mapya ambayo Serikali inayafungua kwa biashara za kitaifa na kimataifa na zile za Uwekezaji Mkubwa ambazo huibua ajira kupitia sekta binafsi. Hapa naona nafasi kubwa ya constructive engagement.[3]
  • Karne ya 21 haizalishi tena ajira zinazotegemea Elimu yenye maudhui ya Karne ya 20. Karne ya 21 inategemea matumizi makubwa ya teknolojia katika utoaji wa huduma.[4]
  • Wahitimu waliopata elimu ya sheria yenye maudhui ya karne zilizopita wanahitaji mabadiliko binafsi makubwa, ya kifikra, kimtazamo na ki-mwelekeo. [5]
  • Mhitimu mzuri ni yule anayeacha milango wazi ya kujifunza kutoka kwa wengine.[6]
  • Katika fani ya sheria, moja ya njia ya kuinoa silaha hiyo ni kujisomea kila wakati kwa sababu  sheria na kanuni huwa zinabadilika mara kwa mara. Sio vyeti vyenu vitakavyofanya kazi ya kutoa huduma.[7]
  • Mhitimu mzuri ni yule anayeacha milango wazi ya kujifunza kutoka kwa wengine.[8]

Marejeo[edit | edit source]

  1. https://sacjforum.org/biographies/hon-prof-ibrahim-hamis-juma
  2. https://web.archive.org/web/20230129171740/https://old.tanzlii.org/tz/speech/hotuba-ya-jaji-mkuu-mhe-prof-ibrahim-hamis-juma-kwenye-mkutano-wa-tatu-wa-baraza-kuu-la
  3. https://web.archive.org/web/20230129180938/https://media.tanzlii.org/files/guidelines/2022-12/HOTUBA%20YA%20MHESHIMIWA%20PROF.%20IBRAHIM%20HAMIS%20JUMA,%20JAJI%20MKUU%20WA%20TANZANIA%20KUWAKUBALI%20NA%20KUWAPOKEA%20MAWAKILI%20-%20TAREHE%2002%20DESEMBA,%202022%20DAR%20ES%20SALAAM.pdf
  4. https://web.archive.org/web/20230129180938/https://media.tanzlii.org/files/guidelines/2022-12/HOTUBA%20YA%20MHESHIMIWA%20PROF.%20IBRAHIM%20HAMIS%20JUMA,%20JAJI%20MKUU%20WA%20TANZANIA%20KUWAKUBALI%20NA%20KUWAPOKEA%20MAWAKILI%20-%20TAREHE%2002%20DESEMBA,%202022%20DAR%20ES%20SALAAM.pdf
  5. https://web.archive.org/web/20230129180938/https://media.tanzlii.org/files/guidelines/2022-12/HOTUBA%20YA%20MHESHIMIWA%20PROF.%20IBRAHIM%20HAMIS%20JUMA,%20JAJI%20MKUU%20WA%20TANZANIA%20KUWAKUBALI%20NA%20KUWAPOKEA%20MAWAKILI%20-%20TAREHE%2002%20DESEMBA,%202022%20DAR%20ES%20SALAAM.pdf
  6. https://www.ija.ac.tz/wp-content/uploads/2019/11/HOTUBA-YA-MGENI-RASMI-MAHAFALI-YA-KUMI-NA-TISA.FINAL_.pdf
  7. https://www.ija.ac.tz/wp-content/uploads/2019/11/HOTUBA-YA-MGENI-RASMI-MAHAFALI-YA-KUMI-NA-TISA.FINAL_.pdf
  8. https://www.ija.ac.tz/wp-content/uploads/2019/11/HOTUBA-YA-MGENI-RASMI-MAHAFALI-YA-KUMI-NA-TISA.FINAL_.pdf