Jump to content

Wq/sw/Edward Snowden

From Wikimedia Incubator
< Wq | sw
Wq > sw > Edward Snowden
Edward Snowden

Edward Joseph Snowden (/ ˈsnoʊdən/; amezaliwa Elizabeth City, North Carolina, ni mshauri wa zamani wa ujasusi wa kompyuta wa Marekani ambaye alivujisha taarifa za siri zilizoainishwa kutoka kwa Wakala wa Usalama wa Kitaifa (NSA) ya huko marekani mnamo mwaka 2013, alipokuwa mfanyakazi na mkandarasi mdogo. Ufichuzi wake huo ulionyesha na kuelezea programu nyingi za uchunguzi wa kimataifa, nyingi zinazoendeshwa na NSA na Muungano wa mashirika matano ya ujasusi kwa ushirikiano wa makampuni ya mawasiliano ya simu na serikali za Ulaya, na kuibua mjadala mkubwa kuhusiana na usalama wa taarifa na faragha ya mtu binafsi.

Nukuu

[edit | edit source]
  • Sitaki kuishi katika ulimwengu ambamo kila kitu ninachofanya na kusema kinarekodiwa. Hilo si jambo ambalo niko tayari kuunga mkono au kuishi chini yake.
  • Sijioni kama shujaa kwa sababu ninachofanya ni changu binafsi: Sitaki kuishi katika ulimwengu ambao hakuna faragha na kwa hivyo hakuna nafasi ya ubunifu.
  • Yasiyokuwa na maadili hayawezi kufanywa kuwa na maadili kwa kutumia sheria za siri.