Wq/sw/Ali ibn Abu Talib
Appearance
Ali Ibn Abu Talib (Kar.: علي ابن أبي طالب * mnamo 600 BK Makka - + Januari 661 Kufah / Irak) alikuwa mkwe wa mtume Muhammad, khalifa wa nne wa Uislamu na imamu wa Shia wa kwanza. Alikuwa pia baba wa wajukuu wa pekee wa mtume.
Aheshimiwa na Washia kama mfuasi wa kweli wa pekee wa mtume.
Nukuu
[edit | edit source]Uadilifu
[edit | edit source]- Taji la mfalme ni uadilifu wake mwenyewe.
- Utatawala iwapo nawe utakuwa mwadilifu.
- Uadilifu huangamiza ulafi , uroho na tamaa.
- Ngome ya Utukufu (ya Allah swt) huikinga nchi yenye mtawala mwadilifu.
Shurutisho na shari
[edit | edit source]- Kulazimisha/Kushurutisha kunaifanya akili iwe kipofu.
- Shari kunamfanya mtu awe mwoga wa uadilifu (ataiongopea)
- Uchokozi ni hatua ya kukaribia maangamizi.
- Kinachodhulumu haki ni kule kusaidia vilivyo batilifu.
- Udhalimu kwa mwenye dhiki ni dhuluma kubwa kuliko zote zile.
- Allah swt huharakisha kuanguka kwa wachokozi.
- Ushidi wa mshari ni kushindwa kwa nafsi yake.
- Kustarehe humu duniani kwa fidia ya akhera ni kujidhulumu nafsi yako.
- Kuwakandamiza yatima na wajane kunaleta magonjwa na kupotea kwa ne’ema.
Ulimi na usemi
[edit | edit source]- Mtu amehifadhika chini ya ulimi wake.
- Ulimi mtamu/mzuri hupata marafiki wengi.
- Ulimi wako utasema kile kilichozoeshwa. (Kwa hivyo jihadhari kabla ya kusema).
- Akili ni busara. Akili ya mpumbavu ipo chini ya ulimi wake(anasema kabla ya kufikiri).
- Ulimi ni mkalimani wa akili.
- Ulimi wa mtu ni uzani wake mwenyewe.
- Ulimi unaathari za kuchoma zaidi ya mkuki.
- Usemi wa kweli ni ulimi mtukufu.
- Jihadhari na ulimi, kwani ni sawa na mshale unaoweza kufyatuka kutoka upinde.
- Mtu bila kusema (ulimi useme mema na kukataza mabaya) ni ama sanamu au mnyama.
- Ulimi wa mwenye busara upo akilini mwake (huongea na akili yake na hufikiria zaidi na kusema kwa uchache kwani ni yenye manufaa).
- Kuujaribu (kucheki) ulimi ni afadhali kuliko kulitazama tumbo.
- Yeyote yule asiye uhifadhi ulimi wake basi ataujutia mbeleni.