Wq/sw/George III of the United Kingdom
Appearance
George III (George William Frederick) ( 4 Juni 1738 – 29 Januari 1820 ) alikuwa Mfalme wa Uingereza na Ireland kuanzia tarehe 25 Oktoba 1760 hadi muungano wa nchi hizo mbili tarehe 1 Januari 1801, baada ya hapo akawa Mfalme wa Uingereza na Ireland hadi kifo chake. Sambamba na hilo alikuwa Duke na mteule mkuu wa Brunswick-Lüneburg ("Hanover") katika Milki Takatifu ya Roma hadi kupandishwa cheo chake kuwa Mfalme wa Hanover tarehe 12 Oktoba 1814. Anajulikana kwa kuhudumu kama Mfalme wakati wa Vita vya Mapinduzi vya Marekani, na baadaye wakati wa Mapinduzi ya Ufaransa na Vita vya Napoleon.
Nukuu
[edit | edit source]- Mfalme mwema anapaswa kufanya mapenzi yake kuwa chini ya maslahi ya nchi yake, kwa maana mambo mabaya yakitokea huathiri inchi na watu wake; lakini Fransisko aliongozwa na hisia tofauti na hivo basi, kujipendekeza kwa wafalme wote kulitia sumu akili yake; badala ya kushughulika na mambo ya nchi yake, alijipa raha kabisa, ndiyo sababu shughuli zake zote za kijeshi zilikutana na changamoto mara kwa mara.